Waziri Mkuu Hachukulii Poa.

Waziri mkuu Muheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa anaunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira, ujenzi wa vyoo bora na unawaji mikono. Jana katika ziara yake halmashauri ya wilaya Lushoto amewaambia wanalushoto si vyema kujisaidia vichakani na pia kukosa choo bora kuna madhara makubwa kiafya na akamalizia kwa kusema ‘USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO’.

Pia Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Muheshimiwa Ummy mwalimu jana katika ziara ya Waziri mkuu halmashauri ya wilaya Lushoto amesema sio kila kitu kinahitaji dada kwani magonjwa mengine tunaweza kujikinga kwa kutumia choo bora na kunawa mikono kwa sabuni. Amesisitiza kuwa ifikapo tar 30 Dec 2018 kila kaya iwe na choo bora na kukitumia pamoja na maji safi tiririka na sabuni.